CONTACT SUPPORT
+255 787 888 417/408/409
Tanzania

SHIRIKA LA PRECISION KUUNGANA NA CCBRT KATIKA KUBORESHA HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU

Shirika la ndege la Precisio Air limetangaza kuingia ushirika na shirika lisilo la kiserikali la CCBRT linalohusika na kuzuia ulemavu na kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu.

Ushirikiano huu uliwekwa bayana jana katika makao makuu ya shirika la ndege la Precision Air jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na vyombo vya habari.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Precision Air bwana Patrick Mwanri alisema kuwa ushirikiano huo kati ya Precision Air na CCBRT utakuwa katika mfumo wa ufadhili.
Akitangaza ufadhili huo, bwana Mwanri alisema Precision Air itatoa idadi ya tiketi 120 kwa shirika la CCBRT kwa ajili ya matumizi ya shughuli zake za kuwezesha kliniki katika mikoa mbali mbali na shughuli za kiutawala kwa ujumla.

‘’Tukiwa kama wazalendo, tunalo jukumu la kutunza na kufanikisha mahitaji ya jamii inayotuzunguka na tunaweza kufanya hivyo kwa kutumia huduma zetu kuleta maendeleo chanya katika jamii. Kama inavyoainishwa katika maazimio yetu, “Kuwa shirika la ndege namba moja na chachu ya maendeleo”, tunaamini ushirikianohuu utaleta mabadiliko muhimu kwa jamii yetu kupitia kazi za CCBRT”.

Aliongeza kusema, “ Tunaelewa kwamba kuna vikwazo kadha wa kadha vinavyozuia watu wenye ulemavu kusafiri kutoka mikoa mbali mbali kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu, na ndiyo maana tunaamini ni muhimu kuunga mkono kliniki zinazotembea ili kuwezesha watu wengi kufukiwa na huduma zinazotolewa na CCBRT”.

Akizungumza na waandishi wahabari, Mkurugenzi wa CCBRT, bi. Brenda Msangi alitoa shukrani zake kwa shirika la Precision Air kwa mchango wa tiketi za kusafiria kwa ajili ya kuunga mkono kazi zinazofanywa nje ya Dar es Salaam na shirika hilo la CCBRT.

“Shirika la CCBRT linavyo vituo washirika katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania. Wafanyakazi wa husafiri kwenda kwenye mikoa hiyo ili kutoa huduma kama zile za macho, mifupa, vipimo, ugawaji wa baiskeli kwa ajili ya walemavu. Tukiwa na washirika kama Precision Air tunaamini tunaweza kuwafikia watanzania wengi zaidi ambao wanahitaji huduma zinazotolewa na CCBRT. Pia mchango huu utasaidia katika kupunguza gharama zitokanazo na safari za mara kwa mara kwa ajili ya shughuli za kiutawala wanazolazimika kufanya wafanyakazi wetu, aliongeza Brenda.

Kuhusu Shirika la Ndege la Precision Air

Precision Air ni shirika la umma lililoanzishwa mnamo mwaka 1993 na linatoa huduma za usafiri wa anga kwenda sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Safari zake huanzia makao yake yaliyoko makuu Dar es Salaam kuelekea Arusha, Kilimanjaro, Serengeti, Mtwara, Kahama, Bukoba, Mwanza, Zanzibar, Tabora, Serengeti, Nairobi, Entebbe na makao makuu ya nchi Dodoma. Huduma nyingine zinazotolewa na shirika ni pamoja na huduma za ubebaji mizigo kwa njia ya anga. Hali kadhalika shirika la Precision Air limewahi kupokea tuzo kadha wa kadha kutoka Tanzania Society of Travel Agents, Africa Aviation News Port, Tanzania Leadership Awards, TASOTA, na pia kampuni ni mshirika wa Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Kuhusu CCBRT

CCBRT ni shirila la afya nchini Tanzania linalolenga kuzuia ulemavu, kutoa huduma za afya bora na nafuu, huduma za kuuguza, na msaada kwa watu wenye ulemavu pamoja na familia zao. Hali kadhalika, shirika linalenga kuzuia ulemavu kwa kujaribu kugundua dalili za awali za tatizo kupitia uboreshaji wa mfumo wa huduma za afya ya mama na mtoto.

We are using cookies to personalize and enhance your use of the Precision Air Website. By continuing to use our website without changing your cookie settings, you are agreeing to the use of cookies as set in the Precision Air Privacy Policy.